Mahafala 104 wahitimu katika chuo cha matibabu cha North Coast Medical College.

Jumla ya mahafala 104 katika chuo cha matibabu cha North Coast wamefuzu katika hafla ya kumi na moja iliofanyika katika chuo hicho ijumaa ya tarehe 24 juni mwaka huu.

Mahafala hao waliofuzu ni kutoka vitengo mbalimbali vya kimatibabu ikiwemo wauguzi ,maafisa wa kiliniki na vitengo vyenginevyo  haya ni kulingana na mkurugenzi wa chuo hicho Reuben Waswa.

Waswa amesema mahafala hao wataleta usaidizi mkubwa kwa jamii haswa katika sekta ya matibabu ya nyanjani ikizingatiwa kuna uhaba mkubwa wa wauguzi nchini.

Amesema uwepo wa kituo maalumu cha mafunzo katika chuo hicho kimerahisisha pakubwa utoaji wa mafunzo kazi na kuwajenga wanafunzi kuwa na ujuzi wa kutosha wa kuwahudumia  wagonjwa wanapofika hospitalini.

Aidha Waswa amesema tangu kuanzishwa kwa chuo hicho katika Kunti ya Kilifi kimepeana fursa nyingi kwa wanafunzi  hasa wa eneo hilo kupata mafunzo ya utibabu huku uchumi katika eneo hilo ukionekana kuboreka  na maendeleo kwa ujumla kukithiri.

Amewataka wanafunzi kuzidi kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yao  huku akiwarai wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kujiunga na chuo hicho kupata mafunzo ya kimatibabu.

Marianne Darwinkel mmoja wa madaktari na waanzilishi wa chuo hicho amefurahia kuona wanafunzi kukamilisha masomo yao na kuhitimu licha ya changamoto wanazokumbana nazo.

Kwa upande wao mahafala hao wameelezea kufurahishwa kwa kuhitimu kwao na kuwashukuru wazazi pamoja na walimu kufaulisha safari yao ya masomo katika chuo hicho

https://boltepse.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287