Timu ya kinadada ya voliboli yalalamikia maandalizi duni

download (5)

Timu ya taifa ya kinadada katika mchezo wa voliboli itakayoshiriki kwenye mashindano ya kufuzu kwa michezo ya olimpiki mwaka huu imelalamikia maandalizi mabaya.

Kocha wa timu hiyo Japheth Munala amesikitishwa na hatua ya serikali kutoisaidia timu hiyo licha ya kwamba inastahili kuelekea jijini Yaounde nchini Cameroon, kuiwakilisha Kenya katika mashindano hayo ya kufuzu olimpiki kuanzia tarehe 12-19 mwezi ujao.

Kenya ni baadhi ya mataifa 17 yatakayoshiriki mashindano hayo ambapo mshindi atapata tiketi kuiwakilisha Afrika katika michezo ya Olympiki mjini Rio de Janeiro, Brazil mwezi Agosti mwaka huu.

Mbali na Kenya miongoni mwa mataifa 17 yatakayoshiriki kwa mashindano ya kufuzu ni wenyeji Cameroon, Algeria, Tunisia, Nigeria, Botswana, Msumbiji, DR Congo,Misri na Uganda.

https://boltepse.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287