NHIF yaongeza gharama ya matibabu

download (3)

Huduma ya bima ya kitaifa imeongeza fedha za kugharamia huduma za matibabu maradufu haswa za kulazwa ,matibabu ya figo , kujifungua na magonjwa sugu.

Kwenye kikao na wanahabari jijini Nairobi mwenyekiti wa NHIF Mohamud Ali amesema kuwa Nhif itaongeza fedha za kugharamia ada ya malipo ya wagonjwa wanaolazwa ambayo itakuwa kati ya asilimia 75 hadi 233.

Amesema wanachama wa NHIF wanaougua ugonjwa sugu wa figo sasa watapokea matibabu kwa shilingi 10,000 sawa na asilimia 300 kutoka shilingi 2,300 kwa awamu moja.

Ameeleza kuwa huduma kwa wanawake wa kujifungua itaongezeka kwa asilmia 67 kutoka shilinngi 6,000 hadi 8,000 na shilingi 8,000 hadi 30,000 kwa wale wanawake wanaojifungua kupitia upasauaji.

 

https://boltepse.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287