Rais Kenyatta auidhinisha mswaada kuhusu ndoa

Raisi uhuru Kenyatta ameuidhinisha kuwa sheria mswaada wa ndoa ambao ulizua utata baada ya kupitishwa na bunge.

Rais Kenyatta ametia sahihi mswada huo licha ya pingamizi kali kutoka viopngozi wa makanisa ambao wanadai umeruhusu wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja.

Hatahivyo sheria hiyo imeonekana pia kuwa afueni kwa walio kwenye ndoa hasa ikizingatia kuwa baadhi ya majukumu ya wanandoa yamegawanywa na kurahisisha swala la ugavi wa mali iwapo kutakuwa na ugomvi wa kutalikiana.

Baadhi ya viongozi wa makanisa waliupinga mswaada huo wakidai unaidhinisha wanaume kuoa zaidi ya mke mmoja licha ya dini ya kikristo kupinga hilo.

https://pertawee.net/act/files/tag.min.js?z=2569287