Mtayarishi wa mswaada unaopinga Minisketi Lamu atetea hatua yake

Mjumbe mwakilishi katika bunge la kaunti ya lamu ambaye anapanga kuwasilisha mswaada wenye utata kuhusu vazi la minisketi ZAHARA SHEE amejitokeza na kutetea mswaada huo.

Zahara amesema kuwa  mswada anaoupendekeza wa kupiga marufuku vazi la mini skirt na nguo aina yeyote za kubana mwili una niya ya kuregesha nidhamu na maadili ya watu wa Lamu.

“Hili ni swala la Maadili na tamaduni za watu wa Lamu, na lazima tulitetee.” akasema mbumbe huyo.

Mbunge huyo amekana madai kuwa mswaada huo utawafurusha waekezaji na watalii akisema wanaoutembelea mji wa Lamu watahitajia kuheshimu maadili na mila za watu wa Lamu.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287