Wachuuzi wa soko la Marikiti Nairobi walalamikia ada ya juu

Shughuli katika soko la Marikiti jijini Nairobi zimetatizwa jumanne asubuhi, baada ya wachuuzi wa bidhaa za reja reja kufanya maandamano na kufululizi hadi nje ya afisi ya Naibu wa Rais William Ruto, kupinga ada wanazotozwa na serikali ya kaunti hiyo.
Wachuuzi hao wanadai kuwa serikali ya Gavana Kidero imeongeza maradufu ada wanazowatoza, licha ya kilio chao cha kuwepo kwa mfumuko wa bei za bidhaa na kuendelea kudorora kwa uchumi wa taifa hili.
Hii sio mara ya kwanza kwa wachuuzi hao kuandamana kupinga ada hizo mpya zinazotozwa na serikali ya kaunti ya Nairobi.
Miezi michache iliyopita, wachuuzi hao waliandamana hadi nje ya afisi ya Gavana Kidero ingawa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na pande zote husika.
https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287