Mtoto Satrin Osinya atoka hospitali
Hatimaye Mtoto Satrin Osinya ametolewa hospitalini leo baada ya kufanyiwa upasuaji yapata majuma mawili yaliyopita ambapo alitolewa risasi iliyokuwa imekwama kichawani.
Osinya alifanyiwa upasuaji huo na kundi la madaktari na kutolewa risasi hiyo ambayo ndio pia ilimuua mamake wakati wa shambulizi kwenye kanisa moja eneo la Likoni mwezi uliopita.
Madaktari waliomfanyia upasuaji mtoto huyo hata hivyo wamesema kuwa ataendelea kuwa chini ya uangaizi huku akiendelea kupata matibabu anapokuwa nyumbani.
Mtoto huyo alioenekana mchangamfu wakati akitoka hospitalini akiwa amebebwa na babake.
Na Asha Bekidusa