Idadi ya Watalii yapungua kutokana na tishio la kigaidi
Bodi ya kitaifa ya utalii nchini imesema kuwa idadi ya watalii wanaozuru humu nchini imepungua pakubwa hasa kutokana na tishio la ugaidi.
Akiongea jijini Nairobi mwrenyekiti wa Bodi hiyo Murithi Ndegwa amesema kuwa idadi hiyo imepungua pakubwa kuanzia mwezi Novemba mwaka uliopita.
Ndegwa ameleezea kuwa idadi ya watalii wa humu nchini pia imepungua pakubwa kutokana na tatizo hilo huku ndegwa akisema kuwa hali hiyo itaathiri pakubwa uchumi wa taifa hili.
Haya yanajiri siku chache baada ya bodi hiyo ya utalii kuwahakikishia usalama watalii wote wanaopania kuzuru taifa hili.
Tayari baadhi ya mataifa yakiwemo Uingereza na Australia yametahadharisha raiya wake kutozuru maeneo fulani kwa hofu ya mashambulizi.
Na Meshak Keicha