Idara ya usalama yakosolewa kuhusu oparesheni yake Eastleigh
Tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu imeikosoa hatua ya inspecta generali wa polisi David Kimaiyo ya kuzuru uwanja wa Kasarani hapo jana na kuitaja kama njia ya kujitafutia umaarufu kwa vyombo vya habari.
Kamishna wa tume hiyo, Susan Chivusia amesema kuwa washukiwa wanaozuliwa katika eneo hilo wanaishi katika mazingira duni huku waume, wanawake na watoto wakichanganywa katika sehemu moja.
Chivusa ameongezea kuwa raia hao wananyimwa haki zao za kibindamu ikiwemo kuzungumza na familia zao.
Serikali aidha imesisitiza kuwa oparesheni hiyo iliyoanzishwa na serikali hailengi jamii wala dini yoyote.
Na Solomon Zully