Rais Kenyatta akutana na mabalozi wa mataifa manne ya magharibi
Rais Uhuru Kenyatta amekutana na kufanya mashauri na mabalozi wanne wa mataifa yenye ushawishi mkubwa ulimwenguni kutoka magharibi.
Mazungunmzo hayo na mabalozi wa Uingereza Dr Christian Turner, mwenzake wa Marekani Robert Godec, na mabalozi wa Australia Geoff Tooth na Canada David Angell katika ikulu ya Nairobi, yameangazia maswala ya kiusalama haswa tishio la ugaidi.
Mabalozi hao wamemhakikishia rais Kenyatta kuwa mataifa yao yataiunga mkono Kenya katika vita dhidi ya ugaidi hususan kwa kuhakikisha kuwa wana usalama wanapata vifaa vya kisasa ili kuweza kukabiliana na mipango ya magaidi.
Wanne hao wamesema kuwa shehena ya mabomu iliyonaswa hivi majuzi mjini Mombasa ni dhihirisho tosha kuwa wanamgambo wa alshabab ni tisho kubwa na wanaweza kusababisha maafa makubwa.