Vifaa vya kutengeza mabomu vyanaswa Eastleigh
Polisi jijini Nairobi wanadai kunasa vifaa vya kutengezea mabomu katika mtaa wa Easteigh usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa polisi jijini humo Benson Kibue amesema kuwa vifaa hivyo vimenaswa katika mtaa wa barabara ya saba mjini humo wakati wa msako wa kuwatafuta washukiwa wa ugaidi.
Kibue amesema kuwa mwenye nyumba ambako vifaa hivyo vimepatikana ametoweka na polisi wanamsaka huku stakabadhi zilizonaswa katika nyumba hiyo zikionyesha kuwa ni mkimbizi kutoka kambi ya Daadab.
Zaidi ya watu elfu moja wametiwa mbaroni mwishoni mwa wiki pekee huku polisi wakisema kuwa msako huo utaendelea hadi pale usalama utakapo imarika.
Viongozi wa jamii ya wasomali hata hivyo wamekashifu oparesheni hiyo ya polisi wakidai inalenga jamii moja, huku polisi wakiitumia oparesheni hiyo kuwapora raia wasiokuwa na hatia.