Rais Kenyatta kukatiza ziara yake ya ughaibuni

Rais Uhuru Kenyatta huenda akakatiza ziara yake ya mataifa ya magharibi ili kuregea humu nchini kuhudhuria sherehe za kufuzu kwa makurutu wa vikosi vya polisi siku ya ijumaa.

Msemaji wa Ikulu Manoa Esipisu amesema kuwa hafla hiyo ni muhimu hasa ikizinmgatiwa tatizo la kiusalama linaloshuhudiwa humu nchini hivi sasa.

Haya yanajiri licha mahakama kutoa agizo la kusitishwa kwa sherehe hizo hadi pale makurutu hao watakapothibitishwa kuwa wamehitimu kuchukua majukumu ya kiusalama.

Takriban makurutu elfu saba watahitimu katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye chuo cha mafunzo ya polisi cha Kiganjo.

Rais Kenyatta yuko ziarani katika mataifa ya Ubelgiji, Uturuki, Rwanda na Uingereza, ziara ambayo itamchukua majuma mawili.

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287