Raila aipongeza serikali kwa kuanzisha mpango wa vitambulisho kwa wakenya walioko nje.
Kinara wa Cord Raila Odinga ameipongeza hatua ya serikali ya Jubilee kuanzisha mpango wa kuwapa vitambulisho wakenya wanaoishi ughaibuni.
Akizungumza katika eneo la Lowell Massachusetts nchini Marekani ambako yuko ziarani, Raila amesema kuwa zoezi hilo litawasaidia wakenya wengi wanaoishi ughaibuni hasa wale ambao wangependa kushiriki uchaguzi mkuu ujao.
Siku ya ijumaa balozi wa Kenya nchini Marekani Jean Kamau alitangaza kuwa serikali itaanza mpango wa kuwapa vitambulisho vya kitaifa raia wote wa kenya ambao wanaishi Marekani na Mexico.
Zoezi hilo linatarajiwa kufannyika april 14 mwaka huu.