Raila akana kujenga jumba la shilingi bilioni moja huko Kisumu
Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, amekanusha madai kwenye gazeti moja la humu nchini kuwa anajenga makaazi mapya kwa gharama ya shilingi bilioni 1 mjini Kisumu.
Msemaji wa Raila, Dennis Onyango amesema kuwa jengo lilalosemekana ni makao makuu ya wakfu wa Raila na wala sio makaazi ya Raila.
Jengo hilo ambalo liko mkabala na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kisumu lnasemekana kuwa na vyumba 70.