Wafanyibiashara wakashifu kunadiwa bidhaa zao katika bandari ya Mombasa
Wafanyibiashara mjini Mombasa wamekashifu vikali utaratibu unaotumiwa hadi kunadiwa bidhaa katika bandari ya Mombasa wakiutaja kuwa kinyume cha sheria.
Mwakilishi wa wafanyibiashara hao Antony Muraya amesema kuwa wameghadhabishwa na jinsi mali yenye thamani ya shilingi milioni 100 ilivyo uza bila ya kuwahuisha kwenye mnada huo na kupelekea mali hiyo kuuzwa chini ya kiwango ambacho wafanyi biashara hao wangeinunua.
Wakati huohuo wafabiashara hao wameitaka serikali kuingilia kati na kuwachunguza viongozi wa mamalka ya mapato nchini pamoja na shirika la ukadiriaji wa ubora wa bidhaa KEBS maana ndio wanaoidhinisha minada hii kwa manufaa ya baadhi ya mabwenyenye wa jijini Mombasa