Kenyatta kuzuru Tanzania Jumatatu

Raisi uhuru kenyata jumatatu atafanya ziara rasmi ya siku mbili mjni Arusha nchini Tanzania ambako anatarajiwa kutoa hotuba muhimu katika bunge la Afrika mashariki siku ya jumanne.

Rais Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa jumuia hiyo anatarajiwa kusafiri kwa barabara hadi Arusha ambapo atakutana na viongozi wenzake wa jumuiya ya Africa mashariki kabla ya kulihutubia bunge la jumuiya hiyo siku inayofuata.

Miongoni mwa maswala yanayotarajiwa kujadiliwa ni miradi ya  miundo msingi, usalama na biashara baina ya mataifa ya jumuiya hii.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287