Seneta Miraj atangaza fursa za ufadhili wa masomo

ULIMWENGU Leo unapoadhimisha Siku ya elimu duniani maarufu kama International Day of Education , Seneta maalum wa kaunti ya Mombasa kupitia chama cha UDA Miraj Abdillahi kupitia wakfu wa Mama Haki Foundation ametangaza fursa  za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi werevu wanaotoka famillia zisizojiweza.

wanafunzi ambao walizoa alama 350 na zaidi katika mtihani wa kitaifa wa KCPE wa mwaka Jana sasa wanaweza kutuma maombi yao kupitia kiunganishi maalum (link) katika mtandao wa google ili kuwasilisha maombi yao.

Ufadhili unatolewa chini ya mpango wa Mtoto Asome Initiative ambao mwaka huu unalenga kufadhili jumla ya wanafunzi 12,wanafunzi wawili kutoka kila eneo bunge la kaunti ya Mombasa.

 

 

Katika mwaka uliyopita wa 2023 mradi huo uliwezesha kufadhili jumla ya wanafunzi 40.

Huku 16 waliyopokea Ufadhili kamili katika shule za kitaifa waliapata alama ya “A” na wengine 22 kwa usaidizi wa wazazi wao katika shule nyengine za upili pia walifanya vyema.

 

Hata hivyo kwenye ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya elimu duniani Seneta maalum Miraj Abdillahi amedokeza kwamba amewasilisha mswada wa uangalizi na ulinzi katika bunge la seneti unaonuia kutoa fursa kwa wanafunzi waliyopachikwa mimba kuregelea masomo yao na kubadili mustakabali wao.

 

Mswada huo unalenga kutoacha mtoto yoyote nyuma na kuhakikisha wanapata fursa ya kuendelea na masomo.

 

 

Seneta miraji vile vile amesisitiza haja ya kuwekwa juhudi za pamoja miongoni mwa wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kike na wenzao wa kiume zinapata ufumbuzi.

 

 

Kwa Mwanafunzi yeyote aliyefaulu abonyeze na kufwata masharti aliyoagizwa ili kupata Ufadhili huu.

https://forms.gle/u6DDUqbqDg6jZxPr6

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287