Mahafala 250 wafuzu chuoni North Coast

Jumla ya mahafala 250 katika chuo cha matibabu cha North Coast wamefuzu katika hafla ya kumi na nne iliofanyika katika chuo hicho ijumaa ya tarehe 24 juni mwaka huu.
Mahafala hao waliofuzu ni kutoka vitengo mbalimbali vya kimatibabu ikiwemo wauguzi ,maafisa wa kiliniki na vitengo vyengine.


Akiongea katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye ni waziri wa Afya katika kaunti ya Kwale Francis Gwama amewataka mahafala hao kutumia vyema elimu waliyoipata katika chuo hicho.
Gwama akiwarai wasiwe na lazima ya ajiza za serikali ambazo kwa sasa ni changamoto na badala yake kutafuta ajira katika sekta binafsi za afya pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali yanayoshughulika na maswala ya afya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo hicho Reuben Waswa amewapongeza mahafala hao huku akiweka wazi mipango yao ambayo wamepanga kuyatimiza.
Wiswa akisema wanampango wa kuanzisha somo la ujasiriamali ambalo litawajenga wanafunzi na elimu ya kibishara,kuanzisha somo la ukunga miongoni mwa masomoso na mipango mengine.

Kenethy Ireri mmoja wa wakurugenzi katika chuo hicho amesema wanajitihidi kuhakikisha wanafanikisha malengo ya chuo hicho na kutoa wanafunzi waliobobea ambao wataenda kuisaidia jamii katika maswala ya utabibu.

https://moonoafy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287