Shedrack Okindo aahidi kuimarisha chama cha UDA Mombasa iwapo atachaguliwa mwenyekiti.
Mwaniaji wa nafasi ya mweyekiti katika chama cha UDA kaunti ya Mombasa Shadrack Okindo ameahidi kumaliza mizozo ya viongozi mbalimbali ambayo yamemekuwa yakishuhudiwa katika chama hicho iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti katika uchaguzi wa chama unaotarajiwa kufanyika tarehe tisa mwezi wa December.
Akiongea na waandishi wa habari katika enoeo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa Okindo amesema mizozo hiyo inayoshuhudiwa imechafua na kudunisha hadhi ya chama hicho tawala.
Okindo akisema bila ya umoja na heshima miongoni mwa viongozi hakuna maendeleo ambayo yatashuhudiwa katika chama hicho.
Aidha Okindo amewaomba wafuasi wa UDA kujiandikisha kwa wingi kuwa wanachama ili kupata fursa ya kumpigia kura kama mwenyekiti sawia na kushirikiana na raisi wiliam Ruto kutekeleza ajenda zake kwa wananchi.
Vilevile ameahidi kuhudumia kila mtu bila ubaguzi iwapo itachaguliwa.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa nafasi ya mwenyekiti katika chama cha UDA kaunti ya Mombasa Zuwena Moses amewataka wafuasi na viongozi wa chama cha UDA kudumisha amani na kuungana ili kuendeleza ajenda za chama hicho.
Zuwena akiwarai wakaazi wa Mombasa kujiunga na chama hicho akisema nafasi zipo wazi kwa mtu yule.