Viongozi Pwani wakashifu semi za seneta wa Nyeri kuhusu mashambulizi kaunti ya Lamu.
Viongozi mbalimbali wa Lamu kutoka katika vuguvugu la watu wa Kunti ya Lamu wamelaani vikali matamshi yaliyotolewa na seneta wa Nyeri Wahome Wamatinga kwamba gavana wa Lamu Issa Timamy anahusika na mashambulizi ya kigaidi yanayoshuhudiwa katika kaunti hiyo.
Wakiongea na waandishi wa habari katika kaunti ya Mombasa wakiongozwa na wakili Yusuf Abubakar amesema maneno hayo hayana ukweli wowote na yamezungumzwa kwa nia ya kuleta chuki na kuharibu Amani ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika jamii za Lamu.
Wakili yusuf akiitaka serikali kuwachukulia hatua viongozi wanaosambaza maneno ya uchochezi katika kaunti hiyo.
Aidha Yusuf amemtaka seneta Wamatinga kukoma kuingilia maswala ya kaunti ya Lamu na badala yake ashughulike kuhudumia wananchi wa Nyeri.
Viilevile amemtaka seneta Wamatinga kumuomba msamaha gavana wa Lamu na wananchi wa Lamu kwa matamshi hayo.
Kwa upande wake naibu mwenyekiti wa wakfu wa Lamu Hassan Albeity amesema kauli ya seneta Wamatinga itahujumu maendeleo,amani na uchumi katika kaunti hiyo.
Albeit akiitaka serikali kupitia Kwa Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki kuingilia kati na kuhakikisha hali ya amani na usalama inarudi kama awali.