Michuano ya Ali Mbogo Super Cup yang’oa nanga kwa kishindo.

Michuano ya Ali Mbogo Super Cup yameanza rasmi hii leo katika uwanja wa Kadongo eneo bunge la Kisauni  huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi kushuhudia mechi ya ufunguzi kati ya PSG dhidi ya B13.

Michuano hiyo inayojumuisha timu 16 kutoka wadi tatu za Junda,Mjambere na Magogoni imefunguliwa rasmi na mdhamini wake muheshimiwa Ali Mbogo ambaye ni mwenyekiti wa mradi wa LAPSET na aliyekuwa mbunge wa kisauni kwa kukabidhi seti za jezi na mipira miwli kwa kila timu inayoshiriki michuano hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya ufunguzi rasmi, Mbogo amesema michuano hiyo imelenga kuwaleta wakaazi wa kisauni pamoja licha ya tofauti za kisiasa ambazo zimekuwa zikishuhudiwa.

Mbogo akisema ni wakati muafaka sasa wakutupilia mbali tofauti za kisiasa na kujumuika pamoja kudumisha amani huku akiwataka viongozi waliomamlakani kuwafanyia wananchi kazi.

Aidha Mbogo amesema kuwa timu itakayoebuka mshindi wa michuano hiyo na kujishindia kitita cha shilingi laki moja na elfu hamsini amewarai wazitumie vyema pesa hizo  kwa kutimiza baadhi ya malengo ya timu hiyo,akiongeza kuwa timu nyingi zimeshindwa kulipa malipo ya kushirika ligi ya FKF kwa kukosa ufadhili na badala yake kushindwa kuendelea na michuano hiyo.

Mbogo pia amesema tayari amefanya mazungumzo na wasaka vipaji maarufu kama scouts kutoka katika baadhi ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya Kenya KPL kuhudhuria michuani hiyo ili  kutambua na kuchukua baadhi ya wachezaji watakaoonysha viwango bora na kuwaendeleza kisoka katika timu zao.

 

 

Mbogo ameweka wazi kuwa michuano hiyo ni miongoni mwa njia moja ya kuwaepusha vijana kushiriki katika vitendo vya uhalifu,kujiunga na magenge na kujiingiza katika utumizi wa mihadarati.

 

Mechi ya ufunguzi imeishia  kwa timu za PSG na B13 kufungana moja moja.

Goli la PSG likitiwa kimiani na Simba huku B13 wakijifunga kupitia mchezaji wao Mody Kibalanta.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287