Maonyesho ya kilimo Mombasa 2023 yangoa nanga.

Mwenyekiti wa maonyosho ya kilimo katika kaunti ya Mombasa Anisa Abdallah amewataka wakaazi wa Mombasa na Kenya kwa jumla kuhudhuria maonyesho hayo kwa idadi kubwa.

Akiongea katika misa ya mavuno ya kutoa shukran katika kanisa la ACK DIOCESE MOMBASA Anisa amesema kuanzia jumatatu milango itafunguliwa ili kuanza kwa shughuli hiyo.

Anisa amewashkuru wadhamini wote ambao wamejitokeza katika ghafla hiyo ambao walitoa vyakula na nafaka mbalimbali kwa dhumuni la kuwasaidia wasiojiweza akiwarai kudumisha ushirikiano huo ili kunufaisha shughuli hizo miaka ya mbeleni.

 

Kwa upande wake Askofu Alphonce Mwaro Baya ameishkuru kamati andalizi ya maonyesho ya kilimo ya mwaka huu akisema ni baraka kuona maonyesho hayo yanafanyika kipindi ambacho mavuno yanapatikana kwa wingi.

Aidha ameiomba serikali kuingilia kati na kudhibiti bei bidhaa na nafaka ili mkulima kuweza kufaidi kutokana na mapato ya uuzaji wa nafaka na mazao hao.