Wakaazi pwani wahimizwa kuhudhuria kwa wingi maonyesho ya kilimo ya Mombasa

HUKU zikiwa zimesalia siku nne  kwa kuanza rasmi maonyesho ya kilimo ya Mombasa mwaka huu,wakaazi wa ukanda wa pwani na Kenya kwa ujumla wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kufaidika na maonyesho hayo.
Akiongea na waandishi wa wahabari katika makao makuu ya ofisi zao baada ya ziara ya ukaguzi wa maatayarisho ya maonyesho hayo,mwenyekiti wa maonyesho hayo Bi Anisa Abdallah amewaomba wakenya kuhudhuria maenyesho hayo kwa wingi huku akiwahakikishia usalama wao wakati wa ziara zao.
Anisa akiwataka wafanyibiashara kuekeza Zaidi katika biashara zao hazwa katika kipindi hiki cha maenyesho ya kilimo kwani kutashuhudiwa wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi.
Aidha Anisa amewarai walimu na wakuu wa shule kuwapeleka wanafunzi kuhudhuria maonyesho hayo kwani yana manufaa makubwa sana kwao ikizingatiwa yanaendana na mfumo wa masomo wa mtaala wa umilisi.
Anisa amesema kufikia sasa tayari shule elfu moja kutoka ukanda wa pwani wamethibitisha kuhudhuria maonyesho hayo,huku wakitarajiwa kunufaika na maswala ya sekta mbalimmbali ikiwemo,kilimo,ufugaji na miongoni mwa sekta nyenginezo.
Kwa upande wake mmoja wa viongozi was  Jumuiya ya kaunti za Pwani ambaye pia alikuwa naibu gavana wa Kilifi Gideon Saburi amesema atashirikiana na mwenyekiti wa maonyesho hayo Bi Anisa Abdallah ili kuhakikisha wanarudisha hadhi ya maenyesho hayo kama yalivyokuwa hapo awali na  kuvutia makampuni na wageni Zaidi katika maenyesho hayo.
Saburi pia amewarai wakaazi wa pwani kujikita katika maswala ya kilimo na ufugaji ili kukuza uchumi wa ukanda wa pwani na kuweza kujikimu kimaisha.
Maonyesho hayo ya kilimo yataanza tarehe sita na kukamilika tarehe kumi huku Rais William Ruto akitarajiwa kuyafungua rasmi tarehe saba.
https://tobaltoyon.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287