EACC yawataka wafanyikazi wa umma kutohofia matamshi ya Waziri Kuria

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imesisitiza kuwa hakuna afisa yeyote wa umma au taasisi ya serikali itakayochukuliwa hatua za kisheria kwa kuhusika na maswala halali na mashirika mengine ikiwemo kuyapatia zabuni.

Msemaji wa tume hiyo Erick Ngumbi amebainisha kuwa kifungu cha 227 kwenye katiba ya Kimeainisha mfumo wa utolewaji wa zabuni unafaa kuwa na usawa, uwazi na wenye ushindani, hivyo haipaswa kwa mtu au shirika lolote kunyimwa zabuni endapo litazingatia vigezo hitajika vilivyowekwa.

Kulingana na Ngumbi tume hiyo ina wajibu wa kisheria kushauri taasisi za umma na maafisa wake kuhusiana na maadili na uongozi katika utendakazi wa majukumu yao ikiwemo kuhusu swala la ununuzi wa bidhaa na huduma serikalini.

Wakati huo huo msemaji huyo amewarai maafisa wa umma serikalini kufuata sheria zinazoongoza uangalizi wa maswala ya umma, ikiwemo kuzingatia matakwa ya sura ya sita ya katiba ya Kenya pamoja na kifungu cha sheria ya uongozi wa maadili ya mwaka 2012.

Haya yanajiri kufuatia kauli iliyotolewa na waziri wa biashara na viwada nchini Moses Kuria akiwaonya maafisa wa umma kwenye mashirika ya serikali dhidi ya kutoa matangazo ya biashara kwa shirika moja la habari nchini.

https://kukrosti.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287