Wavuvi likoni wanufaika na msaada wa vifaa vya uvuvi kutoka serikali ya kaunti ya Mombasa

 

SERIKALI  ya kaunti ya Mombasa kupitia idara ya uchumi samawati, kilimo na ufugaji imetoa vifaa vya uvuvi kwa bodi sita za BMU eneo bunge la Likoni katika hatua inayolenga kuwawezesha wavuvi wa eneo hilo kuendeleza shughuli zao za uvuvi  kwa ufanisi zaidi.

Vifaa hivyo ambavyo vimezinduliwa rasmi na gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Shariff Nassir vinajumuisha majokofu ya kuhifadhia samaki pamoja na mizani za kisasa za kupima miongoni mwa vifaa vengine ambavyo vinatarajiwa kuwapiga jeki wavuvi hao sawia na  kuwaongezea kipato.

Hatahivyo akihutubia wavuvi na wakaazi waliyojitokeza kwenye hafla ya uzinduzi huo gavana Abdulswamad Sharif Nassir amedokeza kuwa kufikia sasa serikali ya kaunti ya Monbasa imebadilisha jumla ya Bodi 12 kati ya 16 za BMU kuwa vyama vya ushirika,katika hatua inayolenga kuwawezesha wavuvi kujiimarisha zaidi kiuchumi.

kuhusu na malalamishi yaliyoibuliwa na wavuvi wa eneo hilo ya kunyakuliwa kwa ardhi mahususi za wavuvi baharini, Gavana Nassir ambainisha tayari mahakama ya upeo nchini imetoa uamuzi kuwa ardhi ya yote ya mita 60 kuanzia mahali hati miliki zinapoisha zinamilikiwa na serikali ya kaunti hivyo amemuagiza waziri wa uchumi samawati kubainisha maeneo hayo yaliyonyakuliwa ili yaregeshwa kwa wavuvi.

Mbali na hayo gavana huyo ameikosoa hatua ya halmashauri ya Bandari nchini KPA kutaka kuliondoa soko la wachuuzi wa samaki la Likoni bila ya kuweka mpango mbadala akisema serikali ya kaunti imekuwa ikiliboresha soko hilo kwa miaka mingi na kamwe haitokubali liondolewa bila ya uwepo wa mpango maalum.

 

Kwa upande wake waziri wa uchumi samawati,ukulima na uvuvi Kibibi Abdallah Khamis amesema vifaa vilivyotolewa vitawasaidia pakubwa wavuvi wa eneo hilo kuepukana na hasara kubwa walizokuwa wakizipata awali ambapo walikuwa wakitumia vifaa vya jadi katika shughuli za uvuvi.

Wakati huo huo waziri huyo amebainisha kuwa mradi huo unatarajiwa kuendekezwa katika maeneo bunge mengine ya kaunti ya Mombasa ili kuhakikisha kuwa wavuvi zaidi wananufaika kutokana na mradi huo ambao pia umefadhiliwa na wizara ya kilimo nchini kupitia mradi wa ASDSP

 

https://omoonsih.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287