Wakuu wa idara za tasnia ya usanii washutumiwa kuwanyasanyasa wasanii

KAMATI ya bunge la kitaifa inayosimamia masuala ya michezo na utamaduni imewashutumu wakuu wa idara zinazosimamia tasnia ya usanii nchini Kwa kuwanyanyasa wasanii na kuahidi kuingilia kati ili kutafuta suluhu muafaka.
Akihutubia wanahabari kwenye kaunti ya Mombasa katika kikao kilichowaleta pamoja wadau wakuu katika tasnia ya usanii na uigizaji pamoja na wasanii, Mwenyekiti wa kamati hiyo Daniel Wanyama ameeleza kutoridhishwa na utendakazi wa wakuu wa idara hizo huku akiwaahidi wasanii kuwa wataanza kupoke marupurupu Yao Kila mwezi kama inavyohitajika kisheria.
Aidha ametaja uongozi mbaya katika idara hizo kuwa changamoto kuu miongoni mwa viongozi hao, huku akibainisha kuwa tayari mipango imewekwa ya kubuniwa kwa mikakati itakayohakikisha kuwa fedha zinazopaswa kulipwa wasanii zinakusanywa pamoja huku Kila msanii akifahamishwa kiwango maalum anachotakiwa kupata Kila mwezi.
Kauli yake imeungwa mkono na mkurugenzi mtendaji wa hakimiliki ya muziki Ezekiel Mutua ambaye ameipongeza kamati hiyo kwa kujenga ushirikiano miongoni mwa wakuu hao huku akiwaahidi wasanii wote kuwa watapata haki sawa katika tasnia hio.