Sarai awapongeza wabunge kwa kupitisha mswada wa fedha 2023

MBUNGE wa Kenya kwenye bunge la Afrika mashariki ambaye pia naibu mwenyekiti wa chama cha UDA Hassan Omar Sarai amewapongeza wabunge kwa kuupitisha mswada wa fedha wa mwaka 2023 uliyopigiwa kura kwenye bunge la kitaifa mnamo siku jumatano juma hilo.
Kulingana Sarai kupitishwa kwa mswada huo kutaiwezesha serikali ya Kenya Kwanza kutimiza ahadi ilizowawekea wakenya wakati wa kampeni ikiwemo kuwawezesha wanaopata kipato cha chini kunufaika na miradi ya maendeleo ya serikali sawia pamoja na huduma bora.
Akitutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kundi la kibiashara la Mombasa links Limited,Sarai aidha amesisitiza kuwa kamwe serikali ya Kenya haitakubali wanasiasa wa mrengo wa upinzani kuhujumu mipango ya serikali ya kuleta maendeleo kwa wakenya, huku akiwarai viongozi hao kubadilisha nia ya kuadaa maandamano baada ya kupitishwa kwa mswada wa fedha.
Mbali na hayo Sarai ameendelea kushinikiza haja ya ushirikiano baina ya viongozi mbali mbali wa kaunti ya Mombasa ili kufanikisha miradi zaidi ya Maendeleo kwa wakaazi wa kaunti hiyo.
Kwa upande wake Seneta maalum wa kaunti ya Mombasa kupitia chama cha UDA Miraj Abdillah amewahakikishia wakenya kuwa serikali itatumia ipasavyo makato ya asilimia 1.5 za hazina ya nyumba ili kuhakikisha kuwa mwananchi wote wanapata kumiliki makaazi yenye hadhi.
Wakati huo huo amepuuzilia mbali madai yaliyoibuliwa na baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa serikali ya Kenya kwanza ndio ya kulaumiwa kufuatia vifo vilivyoshuhuduwa huko Shakahola kaunti katika dhehebu la muhuburi tata Paul Mackenzie, akisema kuwa huu si mda muafaka wa kutupiana lawama na badala take amewataka viongozi hao kushirikiana na serikali ili kutokomeza visa kama hivyo humu nchini.