Awamu ya nne ya wiki ya uvumbuzi pwani yazinduliwa

KITUO  cha Sanaa na teknolojia cha Swahili Pot hub kimezindua rasmi makala ya nne ya wiki ya uvumbuzi pwani PIW yanayotarajiwa kuong’oa nanga mnamo tarehe mbili hadi tarehe sita mwezi Oktoba mwaka huu.

Makala ya awamu hii  yanaandaliwa chini ya kauli mbiu ya kupitisha upeo wa kuwawezesha vijana wanaojipatia kipato kupitia uchumi digitali kwa mustakabali endelevu.

Akihutubia wanahabari wakati wa dhifa ya staftahi ya uzinduzi wa makala hayo mkurugenzi mkuu wa kituo cha Swahili pot hub Mahmoud Noor amedokeza kuwa makala ya mwaka ni ya kipekee kwani yatahusisha wavumbuzi wote kutoka kanda ya pwani katika mataifa ya Afrika Mashariki.

Amesema makala hayo aidha yatatoa fursa zaidi kwa vijana wavumbuzi kwenye kwenye kaunti ya Mombasa na pwani nzima kwa ujumla kudhihirisha miradi yao ili kupata ufadhili sawia na kujitengezea ajira wenyewe.

Wakati huo huo Mahmoud amesisitiza kuwa lengo la wiki ya Uvumbuzi wa pwani ni kusaidia serikali pamoja na mashirika mengine kutatu changamoto wanazokumbana nazo kupitia uvumbuzi mbalimbali unaoasisiwa.

Kwa upande wake waziri wa biashara, utalii na utamaduni kwenye kaunti ya Mombasa Mohamed Osman amedokeza kuwa makala ya mwaka huu yatafungua ukurasa mpya wa ukuaji wa uchumi wa kanda ya pwani Afrika mashariki huku akiwarai wawekezaji zaidi na wafanyibiashara  kujitokeza na kukumbatia fursa hiyo.

wakati huo huo waziri huyo amesema makala ya mwaka huu yatatoa fursa zaidi kwa vijana kujitafutia fursa za ajira zaidi kutokana na bidhaa walizozivumbua.

https://ptirtika.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287