Shahbal ashinikiza mabadiliko ya uongozi katika Chama cha wafanyibiashara KNCCI

MBUNGE  wa kenya kwenye  bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mfanyibiashara maarufu Suleiman Shahbal amesisitiza haja ya mabadiliko katika Uongozi wa chama cha kitaifa cha wafanyibiashara na viwanda KNCCI ili kuwawezesha wafanyibiashara wote chini ya Mwavuli huo kunufaika kikamilifu.

 

Shahbal ameyasema hayo katika mkutano wa wajumbe wa chama hicho wa  kanda ya pwani ambapo alitangaza rasmi kumuunga mkono Daktari Erick Rutto pamoja na mgombe mwenza Mustafa Ramadhan katika wadhfa wa rais na naibu rais wa chama hicho Mtawalia, katika uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa mnamo tarehe nane Mwezi ujao.

 

Wakati huo huo Shahbal alitumia fursa hiyo kuwarai watakaochaguliwa katika kinyang’anyiro hicho kuwaangazia wafanyibiashara wadogo huku akidokeza  kuwa kama mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji katika bunge la Afrika mashariki ataunga mkono jitihada zote za chama hicho katika kupanua wigo wake kwenye biashara ya kikanda.

 

Wakati huo huo Shahbal amedokeza kuwa endapo mpango uliyopendekezwa na Waziri wa Biashara na Viwanda nchini  Moses Kuria wa kuwatoza wafanyibiashara shilingi elfu 5 kama ada ya kujiunga na chama hicho utaafikiwa, basi hakuna budi kuwekwa mikakati muafaka ili kuwawezesha  wafanyibiashara wapya wanaojiunga na chama hicho kunufaika  kikamilifu.

 

Kwa upande wake mgombea wa kiti cha urais katika chama cha KNCCI daktari Erick Ruto ameahidi kutatua  changamaoto zinazowakumba wafanyibiadhara nchini pamoja na kutengeza mazingira rafiki kwa wafanyibiashara ili kuendeleza shughuli  zao bila wasiwasi.

Wakati huo huo Ruto ameahidi kufanya kazi kwa ukaribu na serikali za kaunti na ile ya kitaifa sawia na kuhusisha zaidi wanawake wafanyibiashara ili kuwawezesha kujiendekeza zaidi kiuchumi.

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287