Tawi jipya la Naivas lafunguliwa Bombolulu

SHUGHULI  za kibiashara katika eneo la Bombolulu kaunti ya Mombasa zinatarajiwa kunoga  baada ya duka la jumla la Naivas Kuendelea kutanua  mbawa zake kwa kufungua duka la 94  katika msusuru wa maduka yake nchini kwenye eneo hilo.

Kulingana na msimamizi mkuu  wa mauzo katika duka hilo Willy Kimani, amesema kuwa duka hilo la jipya  litaendelea kuuza bidhaa kwa  bei nafuu ili kunufaisha wananchi wa kawaida  hususan kipindi ambapo gharama ya maisha nchini  imepanda.

Akizungumza na wanahabari Kimani amesema kwa sasa Naivas imefikisha jumla ya maduka 94 kote  nchini  huku  maduka mengine matatu zaidi  katika eneo la Pwani yakitarajiwa kufunguliwa kabla ya kukamilika kwa mwaka huu.

Wakati huo huo  ameirai  serikali ya kitaifa kuweka mazingira bora kwa wafanyibiashara nchini  ikiwemo kuimarishwa kwa usalama sawia na kupunguzwa kwa  gharama ya maisha ili kuwawezesha wananchi  zaidi kununua bidhaa katika maduka ya jumla.

Kwa upande wao  baadhi ya wateja waliojitokeza kununua bidhaa katika duka hilo muda mfupi baada ya kufunguliwa rasmi, wakiongozwa na Kelvin Odoro , wameelezea matumaini ya kuboreka kwa uchumi wa eneo.

Kauli yake imeungwa mkono na  Hamisi Ali muhudumu wa boda boda katika eneo hilo ambaye amesema kuwa kufuatia kufunguliwa kwa duka hilo sasa watashuhudia ongezeko la idadi ya abiria watakaohitaji usafiri huo baada ya kununua bidhaa zao kwenye duka hilo.

 

https://bouhoagy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287