Barayan aahidi kurahisisha utolewaji wa mikopo katika hazina ya Youth Fund

MWENYEKITI wa hazina ya kibiashara ya  vijana nchini  Youth enterprise development Fund Fathma Barayan ameahidi kutatua changamoto na vikwazo vilivyopo katika utolewaji wa mikopo ya hazina hiyo ili kuwawezesha vijana zaidi kunufaika.

Akizungumza katika eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wakati wa kampeni ya kuhamasisha vijana kuhusiana na mfuko was  hazina hiyo , Barayan amewataka vijana katika eneo hilo kutohofia kuchukuwa mikopo hiyo inayotolewa kwani  itawasaidia pakubwa kujiendekeza kibiashara na hivyo  kujiimarisha kiuchumi.

Aidha Barayan amedokeza kuwa mikopo hiyo pia inaweza kutolewa kwa vikundi ambavyo baadhi ya wanachama wake sio vijana endapo asilimia sabini ya uongozi wake utakuwa unajumuisha vijana.

Kadhalika amebainisha  kuwa hazina ya Youth Fund hutoa  mikopo kwa vijana kujitafutia fursa za ajira mataifa ya ughaibuni sawia na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali ili kuwasaidia kuwekeza biashara zao kwa ufanisi baada ya kufanikiwa.

 

 

Vile vile Mwenyekiti huyo amewarai vijana kukataa kuchochewa na baadhi ya wanasiasa kushiriki maandamano ya ghasia na vurugu na badala  yake amewataka kuelekeza nguvu zao katika mambo ya manufaa katika jamii.

Kwa upande wake mshauri wa maswala la kisiasa katika ofisi ya rais Karisa Nzai amewahimiza wakaazi wa eneo la Jomvu kukumbatia fursa hiyo na kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo inayotolewa na hazina ya Youth Enterprise development fund  ili wajiendeleze kibiashara.

Wakati huo huo Nzai amepuuzilia mbali madai ya uwepo wa migawanyiko kati ya viongozi wa chama cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa, akisema kuwa bado wako imara katika kuwahudumia wananchi waliyowachagua katika uchaguzi mkuu uliyopita.

 

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287