Seneta Miraj Abdillahi ampongeza rais Ruto kwa kutoa fursa ya mazungumzo ya pande mbili

SENETA maalum wa kaunti ya Mombasa  kupitia chama cha UDA Miraj Abdillahi amempongeza rais William Ruto na kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya  Raila Odinga  kwa  kutoa fursa ya kuandaliwa kwa majadiliano ya pande mbili  ili kuleta maridhiano ya kisiasa nchini.

Seneta maalum wa kaunti ya Mombasa kupitia chama cha UDA Miraj Abdillahi Akihutubia waandishi wa habari kwenye hafla ya kulizawidi kundi la wanawake la G15

 

Akizungumza katika hafla ya  kuzawidi  chama cha wanawake cha  G15  ambao walihusika  pakubwa katika  kampeni za chama cha UDA  kwenye  kaunti ya Mombasa  wakati wa  uchaguzi mkuu uliyopita, Miraj amesema kuwa hatua iliyoafikiwa baina ya  viongozi hao wawili nchini itasaidia   pakubwa kuendeleza uwiano na mshikamano wa kitaifa.

Aidha Miraj  amelitaka japo lililoundwa kushughulikia mazungumzo  ya pande mbili kuhakikisha kuwa linatumia  fursa hiyo kujadili kikamilifu  maswala yanayowaathiri wananchi wa kipato cha chini.

Kadhalika Miraj  amedokeza kuwa   kufuatia ombi  aliloliwasilisha katika bunge la seneti wiki hii , sekta ya utalii katika kaunti ya Mombasa na pwani nzima kwa ujumla  huenda ikaimarika  kwani ndege zote za kimataifa zitaruhusiwa  kutua katika katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi hivyo kupiga jeki shughuli za utalii sawia na uwekezaji katika eneo hilo.

 

Wakati huo huo amedokeza kuwa kama seneta wa kaunti ya Mombasa kamwe hatasita  kuukosoa uongozi wa kaunti hiyo  endapo utazembea katika kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

 

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287