Makala ya 61 ya KNDFF yakamilika Mombasa
MAKALA ya 61 ya tamasha la kitaifa la maigizo na filamu KNDFF yaliyoandaliwa kwenye kaunti ya Mombasa yamekamilika huku ushindani mkali wa Sanaa ukishuhudiwa baina ya washiriki.
Mashindano hayo yaliyohusisha taasisi za elimu nchini yalifika awamu ya fainali baada ya washiriki bora kuchaguliwa kutoka kwa zaidi ya taasisi 2,000 zilizoshiriki.
Mashindano hayo ya kitaifa yaliyong’oa nanga mnamo tarehe 20 Aprili yaliyowakutanisha zaidi ya wanafunzi 30,000 kutoka taasisi za viwango vyote vya elimu nchini ,waliyochaguliwa kutumbuiza katika halfla ya kilele cha Mashindano hayo iliyofanyika mnamo tarehe 27 na 28 mtawalia mwezi wa Aprili.
Hatahivyo akizungumza wakati alipohudhuria kilele cha Mashindano hayo, waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu ameupongeza ushirikiano baina ya wizara ya elimu na halmashahri ya mawasiliano nchini CA katika kufanikisha tamasha hilo huku akidokeza kuwa wizara yake imeweka mipangilio muafaka ili kuhakikisha kuwa vipaji vya wanafunzi nchini vinakuzwa.
Kwa upande wake katibu wa utawala katika katika halmshauri ya mawasiliano nchini Eric Kiraithe ambaye alimwakilisha mkurugenzi mkuu wa halmashauri hiyo Ezra Chiloba, amedokeza kuwa kama halmashauri watandelea kushirikiana na taasisi nyengine za serikali kufanikisha matamasha kama hayo ili kuunga mkono kikamilifu mipango ya serikali ya kitaifa.
Baadhi ya viongozi wengine serikalini waliyohudhuria tamasha hilo ni waziri wa vijana,michezo na sanaa Ababu Namwamba pamoja na katibu mkuu katika idara ya masomo ya msingi daktari Belio Kipsang.
Itakumbukwa kuwa tamasha hilo linaregea miaka mitatu baada ya kusimamishwa kufuatia ujio wa janga la Covid 19.