Vijana Kisauni kunufaika na michuano ya Akili Kadhaa

HUENDA vijana Katika eneo Bunge la Kisauni Kaunti ya Mombasa wakanusurika kutokana na janga la mihadarati na kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Hii ni baada ya kuzinduliwa Kwa michuano ya kandanda Kwa jina “Akili kadhaa”, inayofadhiliwa na kikundi cha kijamii cha vijana cha Akili Kadhaa, ambacho kinanuia kukuza vipaji miongoni mwa vijana wa eneo bunge la Kisauni.

Akizungumza Wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo Katika uwanja wa Kadongo, mwanzilishi wa wakfu huo ambaye pia aligombea kiti cha uwakilishi wadi wa eneo la Mjambere Katika Uchaguzi mkuu uliyopita, Nuru Sadat amedokeza kuwa michuano hiyo itasaidia pakubwa vijana katika eneo hilo kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira na kuwawezesha kukuza talanta mbalimbali walizonazo.

Aidha kiongozi huyo amebainisha kuwa wanalenga kuendeleza michuano hiyo kila mwaka sawia na kujumuisha  michezo mbalimbali Kwenye mashindano hayo ili kutoa fursa Kwa vijana wengi Katika eneo hilo  kudhihirisha vipaji vyao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa michuano hiyo Juma mashuhuri amesema kuwa anapania kushirikisha timu zaidi katika kaunti ya Mombasa kwenye michuano inayofuata.

Michuano hiyo imeshirikisha timu 16 kutoka ndani na nje ya eneo bunge la kisauni huku ushindani mkali ukitarajiwa kushuhudiwa Kati ya timu zitakazoshiriki.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mamlaka ya ubaharia nchini Hmis Mwaguya amesema watashirikiana na washikidau mbalimbali kuimarisha sekta ya michezo ili kukuza vipaji na talanta mashinani.

 

 

https://atshroomisha.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287