Makala- Ulemavu si hoja
Makala ya Ulemavu si hoja, ni makala inayoangazia safari ya mapenzi ya David Mtsonga na mkewe Joyce Jira ambaye ni mlemavu wa macho. David na mkewe wamevivuka vizingiti kadha wa kadha ikiwemo unyanyapaa katika jamii. Wakithibitisha bayana ukweli wa msemo Mapenzi huota popote na kipendacho moyo dawa, aidha Kipendacho roho hula nyama mbichi.

Licha ya kuwa mumewe si mlemavu wawili hao wamedumu vipi katika ndoa yao? Je, wamefanikisha vipi safari yao ya mapenzi na ndoa?
Fahamu mengi katika makala hii iliyokwenda hewani Jumamosi Disemba 10, 2022