Supkem yataka Azimio kusitisha maandamano Katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan

BARAZA kuu la ushauri Kwa Waislamu hapa nchini Supkem limeikosoa hatua ya Muungano wa Azimio la Umoja one Kenya kuitisha maandamano ya umma kote nchini ikiwa zimesalia siku chache Tu kabla kuanza Kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kulingana na naibu katibu wa kitaifa wa Baraza Hilo Sheikh Sharif Muhdhar Hatamy, maandamano yanayoitishwa na mrengo wa Azimio kamwe hayatatua matatizo yanayokabili Taifa hili Kwa sasa na badala yake huenda yakasababisha maafa zaidi.

Amewahimiza wananchi kupuuzilia mbali mwito wa maandamano unaotolewa na viongozi wa mrengo huo na kuepuka kuchochewa na viongozi wengine wa kisiasa Kwa maslahi yao binafsi.

Naibu katibu wa kitaifa wa SUPKEM Sheikh Muhdhar akihutubia wanahabari Mombasa kuhusu hali ya Taifa.

Wakati huo huo Naibu katibu huyo ametetea nafasi ya viongozi wa dini Katika kuleta uwiano wa kitaifa na amani akisema kamwe hawatasita kutekeleza jukumu Hilo licha shutuma kutoka kwa baadhi ya wanasiasa.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Baraza la Supkem Kaunti ya Mombasa Khalfan Ali amewarai viongozi wa upinzani nchini kubuni mbinu mbadala za kuangazia matatizo yanayokabili Taifa  Kwa njia ya amani badala ya kuitisha maandamano.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Supkem tawi la Mombasa Khatwab Khalifa amewataka viongozi wa upinzani kutoa ushauri utakaoisadia serikali kutimiza agenda zake na kukoma kuchochea wananchi kuhusisha na  maandamano ambayo kulingana naye huenda yakazua ghasia na kutatiza Shughuli maeneo mbalimbali ya nchi.

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287