MAKALA YA HAKI YATOKOMEA
Kulingana na takwimu za kituo cha dharura cha kitaifa kuhusu masuala ya kijinsia
nchini, visa zaidi ya 10,442 vya dhulma za kijinsia viliripotiwa mwaka huu pekee,
ikiwa ni sawa na asilimia 15.
Takwimu hizi zikionyesha wazi kuwa idara husika zilizotwikwa majukumu ya
kupambana na dhulma za jinsia bado hazijawajibika kikamilifu kupambana na
dhulma hizo.
Maswali yakibaki ni wapi wamefeli katika utekelezaji wa majukumu yao?
Takwimu hizo zikionyesha wanafamilia ndio wahusika wakuu wanaotenda
matukio hayo ya dhulma ya jinsia kwa watu wao wa karibu.
Karibu katika makala ya Haki Yatokomea ukiwa nami Yusuf Bakari nkikuelezea ni jinsi gani visa vya dhulma za jinsia vimekuwa vikiongezeka huku watuhumiwa wakikwepa upanga mkali wa sheria wengi kwa kuwa ni watu wenye nacho. Ntakuelezea unyama ambao baadhi ya wazazi wa kiume wamekuwa wakiwafanyia watoto wao wa kike.