Haki yetu yaandaa maandamano kuadhimisha miaka miwili tangu kufurushwa Kwa wakaazi wa Buxton

NA FATHMA RAJAB

SHIRIKA  la utetezi wa haki za kibinaadamu la Haki yetu hii leo limeandaa maandamano ya amani katika jiji la Mombasa  kuadhimisha miaka miwili tangu kufurushwa Kwa wakaazi wa zamani wa nyumba za kupanga za Buxton.

Picha inayoonyesha nyumba za kitambo za buxton

Akihutubia wanahabari wakati wa maandamano hayo afisa wa maswala ya ardhi katika shirika hilo Munira Ali ameutaja mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa za Buxton kuwa uliyotekelezwa Kwa nia ya kuwanufaisha wawekezaji binafsi na wala si kutatua tatizo la makaazi linalonaloikabili Kaunti ya Mombasa.

Wakati huo huo ameishinikiza serikali ya Kaunti ya Mombasa kufanikisha mpango wa ujenzi wa nyumba za kisasa Kwa bei nafuu kama ilivyoainishwa na serikali ya kitaifa, akiitaja  hatua ya serikali ya Kaunti ya Mombasa kutoa zabuni ya ujenzi wa nyumba hizo kwa kampuni binafsi kuwa ilikiuka Sheria na kuchangia pakubwa madhila  Kwa takriban wakaazi 520 waliyofurushwa  Kutoka nyumba hizo.

Aidha ameikosoa tume ya kitaifa ya ardhi nchini NLC na Ile ya maadili na kupambana na ufisadi EACC Kwa kutochukua msimamo dhabiti Katika kulinda na kutetea raslimali za umma dhidi ya kubinafsishwa na wawekezaji wenye maslahi yao binafsi.

Kwa upande wake naibu katibu wa wakaazi wa zamani wa nyumba za Buxton John Tsuma ameonyesha kusikitishwa kwake na jinsi mwekezaji wa mradi huo alivyokiuka maafikiano ya awali aliyowaahidi wakaazi hao. amemtaka muwekezaji wa mradi huo kutoa mpango wa bei nafuu Kwa wakaazi wa zamani wa Buxton ili kuwawezesha kumiliki tena nyumba hizo za kisasa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

https://glimtors.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287