Zaidi ya wanafunzi 50 wapata ufadhili wa sare kutoka kwa mwakilishi wadi ya Kadzandani,Fatuma Kushe.

Zaidi ya wanafunzi 50 wa shule ya msingi na ya chekechea ya Bombolulu Wadi ya Kadzandani Kaunti ya Mombasa wamenufaika na masaada wa sare kutoka kwa Mwakilishi Wadi hiyo Bi Fatuma Swaleh Mote maarufu Fatuma Kushe.

Akiongea wakati wa kutoa sare hizo mapema hii leo, Bi Kushe amekiri kwamba wazazi wengi katika Wadi hiyo wanaishi katika hali ya umaskini na msaada huo utawapunguzia gharama ya sare kwa watoto wao.

Kushe amesema ufadhili huo utaweza kuboresha mazingira bora ya watoto kusomea na kuwatia motisha hata watoto wanaotoka katika familia maskini kusoma kwa bidii wakilenga kutimiza ndoto zao maishani.

Kauli yake imeungwa mkono na Mwalimu mkuu wa shule hiyo wa chekechea na shule ya msingi ya hadi Gredi ya 3 Bi Emily Okumu aliyeiomba Serikali ya Kaunti ya Mombasa kuufufua mradi wa lishe kwa wanafunzi katika shule za chekechea.

 

Kwa upande wao, wazazi wa shule hiyo wakiongozwa na David Juma wameutaja msaada huo kama afueni kubwa kwao kwani wengi wao wameshindwa kumudu sare za shule za watoto wao.

https://ptirtika.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287