Wazazi Mombasa walalamika kuongezwa kwa karo Shuleni

Na ELNORA MWAZO
SHIRIKA la kutetea haki za kibinadamu la Haki Africa pamoja na wazazi katika kaunti ya Mombasa, wameonyesha ghadhabu yao kufuatia hatua ya baadhi ya shule za upili kwenye kaunti hiyo kuwatoza karo ya juu wanafunzi wanaojiunga Na kidato cha kwanza.
Wakiongozwa na Walid Sketi wazazi hao wamedai baadhi ya shule hizo zimeongeza karo kwa zaidi ya shillingi elfu saba kwa kila mwanafunzi huku wakimuomba waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu kuingilia kati Na kulitatua tatizo hilo ambalo kulingana nao wamelitaja kuwa ufisadi.
Vilevile wamelalamikia hatua ya baadhi ya shule kuendeleza masomo ya ziada na kuwatoza wazazi ada ya msomo hayo licha ya waziri wa elimu kuyapiga marufuku katika shule za msingi na Sekondari nchini.
Kwa upande wake Abdallah Mbwana,mwenyekiti wa wakaazi wa mtaa wa old town amemtaka rais William Ruto kuunda jopo la kuthathmini matokeo ya kitaifa ya kidato cha nne KCSE, akidai kuwa matokeo hayo yaligubikwa na udanganyifu mkubwa.