Tume ya SRC yakana mpango wa kuwaongezea wafanyikazi marupurupu

NA MOSES WANJALA

TUME ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma humu nchini (SRC) imekana madai ya kutaka kuwaongezea marupurupu wafanyikazi wa umma.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, tume hiyo imekanusha uwepo wa mpango wa kutoa nyongeza kwa wafanyikazi wa umma, ikiyataja madai hayo kuwa ya kupotosha , wakati huo huo ikionyesha  masikitiko yake na jinsi asasi za serikali zimepotoshwa na taarifa hiyo.

Haya yamejiri kufuatia taarifa zilizokua zimechapishwa katika gazeti la Daily Nation zilizodai kuwa tume ya SRC ilikuwa na mpango wa kuwaongezea maafisa wa serikali marupurupu ya makazi.

Kulingana na taarifa hiyo , wafanyikazi wa umma kwenye kitengo cha K wangepata marupurupu ya Ksh.16500 kutoka Ksh.10000,huku wafanyikazi wanaohudumu katika jiji la Nairobu chini ya kitengo cha A wakipata marupurupu ya Ksh.3750 kutoka Ksh.3000 wanazopokea sasa.

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287