Operation Linda Ugatuzi yaanza kukusanya sahihi Mombasa

NA ELNORA MWAZO

SHIRIKA  la Operation Linda Ugatuzi Limezindua rasmi kampeni ya ukusanyaji wa sahihi kwa wananchi wa kaunti ya Mombasa ili kuliwezesha kubadilisha jumla ya vipengele 30 vya katiba iliyopitishwa mwaka 2010.

Kulingana na Kiongozi wa Operesheni hiyo Proffesor Fred Ogolla Miongoni mwa vipengele vya Sheria Wanavyonuia kubadilisha kutokana na kampeni hiyo ni pamoja na Sheria itakayowalazimu manaibu wa rais kusubiri kipindi cha miaka mitano kabla ya kuruhusiwa kuwania kiti cha urais, Magavana wa zamani kutoruhusiwa kuwania kiti cha Useneta ,Kuazishwa kwa hazina Fedha za kutawisha Wadi sawia kujumuishwa kwa Hazina ya CDF katika katiba miongoni mwa vipengele vyengine vyenye utata.

Ogolla aidha ameonyesha wasi wasi wake kuhusiana tatizo la Mfumuko wa bei za bidhaa na ongezeko la gharama ya maisha linaloenendelea kushuhudiwa katika kanda ya pwani na kenya nzima kwa ujumla, akisema kuwa ipo haja kwa rais William Ruto kuisitisha mara moja hazina ya hasla Fund iliyozunduliwa mnamo mwezi Disemba mwaka jana kwani kulingana naye haina manufaa yoyote kwa wakenya.

Miongoni mwa maswala mengine ambayo amemtaka rais William Ruto kuyaangazia ni pamoja na Kuendeleza miradi amabayo bado haijakamilika sawia na kutowafuta maafisa kazi kiholela maafisa waliyoteuliwa na mtanguzi wake Uhuru Kenyatta.

Wakati huo hupo amewarai wananchi wa eneo la Pwani kushirikiana kwa kutia sahihi mapendekezo hayo ya Kubadilisha baadhi ya Vipengele hivyo vya katiba kwa manufaa yao

https://uwoaptee.com/act/files/tag.min.js?z=2569287