Matokeo ya upasuaji ya mshukiwa aliyefariki ndani ya seli kaunti ya Kilifi yatolewa

Na Rukia Amin

Matokeo ya awali ya upasuaji kuhusiana na kifo cha Kijana aliyefariki katika kituo cha polisi cha Kizurini eneo bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi yamebainisha kuwa marehemu alifariki kutokana na ukosefu wa Oksijeni katika ubongo wake.

Matokeo ya upasuaji huo uliyofanywa chini ya uangalizi wa shirika la kutetea haki za kibinaadamu la Haki Afrika aidha yamebainisha kuwa Santa Nguma mwenye umri wa miaka 34 alikuwa na majeraha katika mwili wake kabla ya kufikilishwa katika kituo hicho cha Polisi japo hayajatajwa kuwa sababu kuu iliyopelekea kifo chake.

Awali taarifa ya idara ya polisi kuhusiana na Kifo hicho ilikuwa imebainisha kuwa mwendazake alijitia kitanzi kwa kutumia blanketi.

Kwa upande wake familia ya mwendazake ikiongozwa na Alfred Mtengo imeitilia shaka taarifa hiyo ya Polisi akisema ni kinaya kwa jamaa wao kufariki kituoni humo ilhali polisi wanajukumu la kuhakikisha usalama wa washukiwa.

Mashirika ya kuteatea haki za kibinaadamu yakiongozwa na Shirika la Haki Africa yameitaka halmashauri ya kusimamia Utendakazi wa polisi IPOA kuingialia kati na kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na kifo hicho ili haki ipatikane familia ya mwenzadake.

Aidha yameshinikiza serikali kuweka kamera za CCTV katika seli za vituo vya polisi nchini ili kuhakikisha usalama zaidi wa washukiwa.

https://ptirtika.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287