UGONJWA WA PID

Takribani asilimia 70 ya Maambukizi ya PID yaani Pelvic Iflammatory Disease
nchini vinasababishwa na ngono zembe kote.
Wataalam wa maradhi hao wanadai kwamba visa hivyo huwa havijulikani na
havina dalili mwafaka.
Kulingana na Data ya mwaka wa 2014 na 2015 inaonyesha kwamba asilimia 7
kutoka kaunti ya Mombasa wameathirika baada ya sampoli 456 kufanyiwa
utafiti huku wasichana wa sekondari na vyuo wakiwa waathiriwa zaidi.
Karibu kwenye Makala donda ndugu la mwanamke jina langu ni Mishi Harun.

PID yaani (Pelvic Iflammatory Disease)ni ugonjwa wa maambukizi kwenye
fupa la nyongo ya wanawake,Maambukizi yanayosambaa katika via vya uzazi
vya mwanamke na kuathiri Nyongo.
Kuna bacteria wa aina nyingi ambao wanaweza kusababisha PID,ila
maambukizi ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi ambapo
bacteria hao huambukizwa wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya
kutumia kinga.
Ugonjwa huu unaweza kuwaathiri wanawake wa umri wowote ila wale
wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24 huathirika zaidi.
Wataalamu wa magonjwa hayo wanaeleza jinsi wanawake wajawazito
walivyohatarini mwa kupoteza ujauzito kutokana na kukosa uwezo wa
kubeba mimba kwa miezi tisa.

Daktari wa shida za uzazi kutoka hospitali ndogo ya Mtwapa kaunti ya Kilifi
Beverlyn mutei anasema japo ugonjwa huo umekuwa ukiwashika kinamama
wengi ila ugonjwa huo hutibika endapo mwathiriwa ataugundua mapema na
kuanza matibabu mara moja.

Baadhi ya wagonjwa walioathirika na ugonjwa huo wanaeleza jinsi
walivyogundua kuathirika na PID na jinsi walivyokuwa wakijitenga na
Jane japo si jina lake halisi,huyu ni mwathiriwa wa ugonjwa wa PID na
anaeleza jinsi ulivyomwathiri kiasaikolojia.

Jane anaeleza jinsi alivyosumbuka kupata mtoto kwa miaka mitatu,akisema
ugonjwa wa PID ndio uliokuwa ukichangia madhila hayo.Ila kwa sasa ni
mwenye tabasamu baada ya kufanikiwa na mtoto kutokana na matibabu
aliyoyapata ya ugonjwa huyo.

Ndoa ya Jane nusra itibuke baada ya kutomuridhisha bwanake kutokana na
maumivu aliyokuwa akiyapata.Kulingana na bwanake Jane ,haikuwa rahisi
akisema hali hiyo ilikuwa ikimpa changamoto kutokana na harufu mbaya
iliyokuwa ikitoka kwa mkewe.
Anasema aligundua mkewe ameathirika na PID baada ya kuzuru hosptalini
kujua harufu na uchungu unaotoka kwa mkewe unasababishwa na nini.

Mwathiriwa mwengine ambaye tutamwita Joyce mwenye umri wa miaka 38
na ambaye mpaka sasa bado hajafanikiwa kupata mtoto kutokana na maradhi
hayo.
Anasema si watu wa mtani tu bali hata familia ya bwanake ilikuwa ikimsema
kutokana na kukosa kupata mtoto huku akiwa na matumaini siku moja ndoto
yake ya kupata mtoto itatimia kutokana na dawa anazoendelea kutumia.

Muuguzi Asia Ahamed anasema kwamba wanawake wenye ugonjwa wa PID
hupata changamoto ya kushika mimba akisema wanawake wenye
changamoto hiyo hufanyiwa utaalamu wa vipimo kisha kupelekwa kwenye
maabara ili kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo wataalamu wanasema kwamba dalili za ugonjwa huu huwa ni
maumivu kwenye nyongo na wakati wa kujamiiana,Kutokwa damu nyingi
wakati wa hedhi,Kutokwa majimaji yasiyo ya kawaida kwenye sehemu za siri
miongoni mwa dalili zengine.
Jamii zimeshauriwa kutafuta matibabu mapema kwani endapo utafuatilia
maelezo ya daktari na dawa basi huenda ukapona na kurudi hali yako ya
kawaida.

Jina langu ni Mishi Harun kwenye Makala ya donda ndugu la mwanamke.

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287