NADIRA MURSAL AIBUKA KIDEDEA KATIKA MTIHANI WA KITAIFA WA SHULE ZA MFUMO WA KCIM

Mwanafunzi Nadira Mursal Mohamed kutoka Shule ya Al Furqan integrated iliyoko  Kaunti ya Wajir ameibuka wa kwanza kote nchini katika mtihani wa kitaifa wa Shule zenye mfumo wa mafunzo ya dini ya kiislamu (Kenya Certificate of intermediate Madrassa Education)

 

Nadira amefanikiwa kujizolea alama 546 kati ya alama 600 akiwa na daraja A huku akifuatwa kwa karibu na Abdirahman Ibrahim  Gelow Wa Shule ya Al Hilal Integrated iliyoko  kaunti ya Garissa aliyezoa alama 523 .

 

Aliyefanikiwa kuibuka katika nafasi ya tatu ni mwanafunzi Hibo Ibrahim Hajir kutoka Shule ya Arrahman Integrated  kaunti ya Nairobi ambaye amekamilisha nafasi ya tatu bora kwa kujizolea alama 520.

Kati ya Shule 18 zilizofanya mtihani huo mwaka huu Shule ya Arrahman Academy kutoka kaunti ya Nairobi imeibuka Shule bora kwa kupata alama wastani ya 456.25 ikifuatwa na shule ya Al Hilal ya Garissa kwa alama wastani 449.52,nayo shule ya Al furqan ikifunga nafasi ya tatu bora kwa kupata alama 449.52.

Hatahivyo akitangaza matokeo hayo mjini Mombasa wakati wa Konagamo la wadau na walimu wa shule hizo,  Mwenyekiti wa baraza la maendeleo ya mtaala wa masomo ya kiislamu nchini ICDC Sheikh Hassan Sugow amedokeza kuwa kuyumba   kwa matokeo ya mtihani huo  mwaka huu kumechangiwa na mabadiliko ya kalenda ya masomo nchini , jambo ambalo  amesema lilitatiza  pakubwa  maandalizi ya  kutosha kwa ajili  ya mtihani huo.

Aidha amesema kuwa ipo haja ya kuwekwa kwa mikakati kabambe ili kuhakikisha kuwa Somo la lugha ya kiarabu linamarika zaidi  hasa ikizingatiwa kuwa matokeo ya somo hilo yameendelea kudorora tangu mwaka 2017 ,akiwatolea  wito walimu na wadau kubuni mikakati muafaka itakayoimarisha matokeo yake siku za usoni.

 

Vile vile  amesema kuwa Wananuaia kutuma fursa ya kongamano hilo la siku tatu kujadili na Kuweka mikakati mbadala itakayowezesha kuboresha mtaalahuo  zaidi kuzivutia shule nyingine hapa nchini kujiunga nao.

 

Mtaala wa masomo hayo unashirikisha shule zilizokumbatia mfumo wa dini na mfumo wa 844 kwa pamoja huku kati ya Shule zaidi ya 300 zilio na mfumo wa dini ni jumla ya shule 18 zilizojisajili kwa mtihani mwaka huu.

 

Miongoni mwa Shule hizo katika kaunti ya Mombasa ni pamoja na Sheikh Zayed, Abu Hureira pamoja na Shule nyenginezo.

https://ptirtika.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287