Wananchi Mombasa Kuumia mgomo wa madaktari ukitatarajiwa kuanza Jumatatu

Huenda huduma za matibabu katika hospitali za Umma kaunti ya Mombasa zikalemazwa kufuatia  Mgomo wa madaktari  unaotarajiwa Kuanza siku ya jumatatu juma lijalo endapo makataa ya siku saba yaliyotolewa na madakatari wa kaunti hiyo  wakishinikiza kulipwa mishahara ya miezi miwili yatamalizika bila ya maafikiano .
Kulingana na Naibu katibu wa Chama cha madaktari KMPDU Kanda ya pwani Ghalib Salim amesema kuwa mbali na kucheleshwa kwa mishahara ya mwezi wa Oktaba  na Novemba , serikali ya kaunti hiyo pia haijakuwa ikilipa makato ya mishahara kwa kipindi cha miezi mitano iliyopita  jambo lilosababisha madaktari wengi kujumuishwa katika taasisi ya CRB.

Kauli yake imeungwa mkono na katibu wa chama cha wanamaabara kaunti ya Mombasa Moses Maingi ambaye amesema kuwa Wahudumu wa afya katika kaunti ya Mombasa wamekuwa wakipitia chanagamoto chungu nzima kutokana na kucheleshwa  mishahara, akisisitiza kuwa hakuna huduma za matibabu zitakazotolewa siku ya jumatatu katika hospitali za umma kama  matakwa yao hayataangaziwa ipasavyo.

Kadhalika wahudumu hao wa afya wamesema kuwa hawatakubali kulipwa mshahara wa mwezi mmoja ili waree kazini ,wakisema ni sharti serikali ya kaunti iwalipe mishahara ya miezi miwili wanayodai.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema kuwa japo madakatari  hao wana haki ya kikatiba kuandaa mgomo, amewataka kutathmini upya uamuzi wao na kutoa fursa ya majadiliano ya kina ili kuzuia athari katika sekta ya afya kwenye kaunti hiyo.

Aidha amebainisha kuwa tangu utawala wake ulipochukuwa hatamu ya uongozi katika kipindi cha siku themanini na tatu pekee wamefanikiwa kulipa malimbikizi ya mishahara ya miezi mitatu sawia na makato yote ya mishahara ya takriban shilingi milioni 365.

kadhalika amedokeza kuwa ni mishahara ya Mwezi Novemba pekee inayodaiwa na Madakari hao,akiwataka kuwa na kwani bado wanasubiri mgao wa fedha kutoka kwa serikali kuu .

Vile vile amesema kuwa tangu aingie mamlakani amechukuwa hatua muhimu kuangazia maslahi ya wahudumu wa afya katika kaunti hiyo.

miongoni mwa hatua alizochukua ni pamoja na kuagiza taasisi ya CRB kuwaondoa madaktari wote wa kaunti hiyo waliyojuishwa awali na taasisi hiyo sababu ya kushindwa kulipa makato yao ya mishahara.

wakati huo huo amedokeza kuwa kama serikali ya kaunti wamekuwa wakiihusia viongoni wa miungano ya madaktari katika mipango na maamuzi yote muhimu yaliychukuliwa na kaunti hiyo

https://pertawee.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287