Wahisani watakiwa kujitokeza na kutoa msaada wa chakula Kwale

Baadhi ya wakaazi waliothirika kutokana na baa la njaa wakipokea chakula cha msaada

Wito umetolewa kwa wahisani kujitokeza na kutoa chakula cha msaada kwa shule ambazo ziko sehemu zilizoathirika  na baa la njaa katika kaunti ya Kwale.

Akiongea baada ya kupokea chakula cha msaada kutoka kwa wakfu wa Rashid Abdallah Supercup,naibu gavana wa kaunti ya kwale Chirema Kombo amedokeza kuwa kuna haja ya kutolewa kwa msaada huo hususana katika kipindi hiki ambapo wanafunzi wanatarajia kuanza mitihani yao ya kitaifa hivi karibuni.

Kombo aidha amebainisha  kuwa chakula hicho cha msaada kilichotolewa  kitasambazwa kwa wakaazi ambao wameathirika na baa la njaa maeno ya kinango na Lunga Lunga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa wakfu wa Rashid Abdhalah supercup Foundation Luiza Kithi ameahidi kushirikiana na serikali ya kaunti ya kwale ili  kuhakikisha familia zinazoathirika na baala la njaa zinasaidika huku akiahidi kuendeleza mradi huo kwa kaunti zengine za kanda ya pwani.

 

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287