Maseneta kujadili upya miswada iliyohitilafiwa na kipindi cha uchaguzi mkuu

Kiongozi wa waliyowengi katika bunge la seneti Aaron Cheruiyot akihutubia kongamano la kamati ya shughuli za bunge mjini Mombasa

Kamati ya shughuli za bunge la seneti nchini imesema iko tayari kuirejesha na kuijadili upya baadhi ya miswada muhimu iliyowasilishwa kwenye bunge hilo na viongozi waliopita.

Akizungumza mjini Mombasa baada ya kulifungua rasmi Kongamano la  kamati hiyo kwa niaba ya spika wa bunge la seneti Amason Kingi, naibu spika Kathuri Murungi, amesema bunge hilo litairejesha upya miswada ambayo haikujadiliwa kikamilifu na bunge lililpotangulia.

Murungi amebainisha kuwa  baadhi ya miswada iliyowasilishwa katika bunge hilo la seneti haikupata fursa kujadiliwa kutokana na kuhitilafiwa na kipindi cha uchaguzi mkuu uliyopita.

Vilevile, naibu huyo wa spika wa bunge la seneti, amesema wataipatia kipaumbele miswada inayoangazia changamoto zinazomkabili mwananchi ikiwemo janga la ukame ambalo linashuhidiwa katika maeneo mbalimbali hapa  nchini Kwa sasa

Aidha amesema kongamano hilo linanuia kutoa mafunzo ya namna ya kuwawezesha tekeleza majukumu yao na kuweka mikakati ya ushirikiano wa kiutendakazi ili  kufanikisha juhudi za kukabili changamoto zinazoshuhudiwa humu nchini.

Kwa upande wake, Kiongozi wa walio wengi katika bunge la Seneti Aaron Cheruyot amesema kuwa wataweka jitihada za kutatua mizozo kati ya bunge  la seneti  na lile la  kitaifa ili kubainisha wazi majukumu ya mabunge hayo na kuepusha migongano iliyoshuhudiwa hapo awali.

https://jouteetu.net/act/files/tag.min.js?z=2569287