MAKALA YA HUJAFA HUJAUMBIKA
Ni kawaida ya wazazi kuwa na matumaini ya kuzaa watoto timilifu lakini ni fumbo kubwa ambalo Mola ametuokea kutojua hali ya motto mpaka pale atakapozaliwa.
Mara nyingi wazazi wanapopata mtoto mwenye mapungufu au ulemavu huwaathiri wazazi kisaikolojia na hata kuwakataa na kuwafanyia uovu japo wapo wengi wanaokubaliana na hali na kuwalea vyema.
Asilimia kubwa ya wazazi wanaozaa watoto wenye mapungufu au ulemavu barani Africa hutengwa na baadhi ya jamaa zao.
Katika Makala yangu ya HUJAFA HUJAUMBIKA nitaangazia baadhi ya madhila ambayo kina mama waliojifungua watoto wenye ulemavu wanapitia.
Madhila ambayo huwaacha wengine kuachwa na waume zao na wengine hata kutengwa na familia na jamii. Licha ya kwenda kwa idara husika kusaka haki kutoka kwa baba wa watoto hao ya kuwasaidia kuwalea inaonekana kuwa ngumu kupata haki hizo.
Visa ambavyo mashirika ya kutetea haki za kibinadamu pamoja na viongozi wa kidini wamevikemea vikali sana hii ni baada ya baadhi ya waathirikiwa kufikia hatua hata ya kuwauwa watoto hao ili kuepukana na fedheha na kejeli za wanajamii.
Fatilia kwa makini Makala haya ili kuweza kupata kujua wanayopitia kina mama hao lakini kaa ukijua hujafa hujaumbika.