Shirika la Samba Sports lahamasisha vijana Mtongwe

Shirika la Samba sport youths Agenda Kwa ushirikiano na Mashirika mengine ya kijamii limeandaa hafla ya maenyesho ya talanta miongoni mwa vijana kwenye wadi ya Mtongwe eneo Bunge la Likoni inayonuia kutoa hamasisho kuhusiana na umuhimu wa kudumisha amani na umoja katika jamii.

Hafla hiyo ambayo imeshirikisha wawakilishi kutoka dini na makabila mbalimbali eneo Hilo pia imetoa fursa Kwa vijana kuonyesha talanta mbalimbali walizo nazo katika Nyanja ya usomaji mashahiri,uigizaji,uimbaji na talanta nyengine nyingi za uvubunifu.

Hatahivyo akizungumza na idhaa ya Radio Salaam kwenye hafla hiyo mwanachama wa Shirika Hilo Juma Ali amedokeza kuwa Chini ya Mradi wa Shared Futures, Shirika la Samba sports limeweka  mpango wa kuhamasisha vijana wa dogo katika taasisi za elimu kuhusiana na umuhimu Kwa kuishi Kwa Umoja Katika kijamii.

Aidha Juma amezitolea wito Serikali za kaunti kushirikiana na Mashirika ya kijamii ili kuhakikisha kuwa vijana wenye talanta mbalimbali kutoka maeneo ya mashinani wanawezeshwa  kikamilifu ili kufikia ndoto zao.

Mradi huo Kwa sasa unatekelezwa katika Kaunti ya Kwale na Mombasa.

https://eechicha.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287